Tanzania,Msumbiji zakubaliana kuanzisha mchakato wa kusainiwa MoU kati ya TIC na APIEX

MAPUTO-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Msumbiji zimekubaliana kuanzisha mchakato wa kusainiwa Hati ya Mkubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya TIC na APIEX.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo, Msumbiji.

Makubaliano hayo yalifikiwa Aprili 3, 2024 wakati Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji alipokutana na Bw. Gil Bires, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kukuza Uwekezaji na Usafirishaji wa Bidhaa za Msumbiji Nje ya Nchi (Investment and Export Promotion Agency - APIEX) kwenye ofisi za wakala huyo jijini Maputo.
Katika mkutano huo, Bw.Bires alikubaliana na pendekezo lililotolewa na Mhe. Balozi Kasike la kuanzishwa ushirikiano huo mapema hasa kwa kuzingatia uhusiano wa kihistoria na ukaribu wa kijiografia baina ya nchi hizi mbili.

Awali, Mhe. Balozi Kasike alieleza kwamba kwa muda mrefu Tanzania na Msumbiji zimekuwa na uhusiano mzuri katika nyanja za kisiasa na kijamii, hivyo ni vyema uhusiano huo ukaelekezwa pia kwenye nyanja ya Kiuchumi ili kusaidia kuleta maendeleo endelevu kwenye nchi hizo mbili.
Katika kutekeleza suala hilo, alisisitiza umuhimu kwa TIC na APIEX kuanza mchakato wa kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) itakayowezesha taasisi hizo pamoja na masuala mengine kurasimisha ushirikiano huo.

Pia, kubadilishana utaalamu na uzoefu, kushirikiana katika kuandaa matamasha na matukio mengine yanayohusu Sekta ya Uwekezaji pia kubainisha maeneo mahususi ya ushirikiano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news