Kampuni za Kitanzania zahimizwa kuchangamkia zabuni Comoro

MORONI-Kampuni za Kitanzania zimetakiwa kuomba kandarasi za ujenzi wa miradi inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa visiwani Comoro.
Hayo yameelezwa wakati wa mazunguzo kati ya Balozi wa Tanzania, Comoro, Mhe. Saidi Yakubu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa, Comoro, Bi.Rejane Hugouneno De Vreyer yaliyofanyika Moroni Machi 12, 2025.
Bi. De Vreyer alimweleza Balozi Yakubu kuwa Shirika lake linafadhili miradi na programu zenye thamani takribani Euro Milioni 113 kwa mwaka katika sekta za Afya, Ujenzi, Tehama na pia kutoa ushauri katika maeneo ya mifumo ya kodi, bajeti na maboresho ya sera.
Alisema kuwa,miradi yote hiyo hutolewa kwa kandarasi za kimataifa na kutoa mwaliko kwa kampuni za Kitanzania kuchangamkia fursa hizo.
Kwa upande wake, Balozi Yakubu alimweleza Bi De Vreyer kuwa Tanzania ina ushirikiano mkubwa na Comoro katika maeneo yote aliyoyazungumzia na kwa hivi sasa wamekwishaanza kualika kampuni za Kitanzania kuchangamkia fursa za zabuni zinazotangazwa visiwani Comoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news