Waziri afurahia uwepo wa NHIF maonesho ya OSHA

SINGIDA-Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amefurahishwa na uwepo wa banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwenye Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi.
Akitembelea mabanda ya Maonesho katika Viwanja vya Mandewa Mkoani Singida, alisema amefurahishwa na uwepo wa NHIF kwa kuwa huduma inazotoa zinahitajika na kila mwananchi.

"NHIF safi sana kwa uwepo wenu, endeleeni kuwaelimisha wananchi ili wajiunge na wawe na uhakika wa matibabu wakati wote," alisema Mhe.Ridhiwani.
NHIF imekuwa ikishiriki katika maonesho mbalimbali ambapo kwa sasa inahamasisha na kutoa elimu ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ili kila mwananchi ajiunge na awe na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha.

》BIMA YA AFYA KWA WOTE, JIUNGE SASA》

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news