ARUSHA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Anga.

Amesema kuwa moja ya eneo ambalo Rais Dkt. Samia ameendelea kusimamia ni ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege nchini ikiwemo ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha msalato kilichopo jijini Dodoma.

“Pia tunaendeleza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti unaolenga kukuza utalii wa mazingira huku tukihifadhi mfumo ikolojia wa Serengeti.”

Amesema kuwa kutokana na jitihada mbalimbali za Serikali za kuiimarisha Sekta ya anga, Tanzania imetajwa na Shirika la ICAO kushika nafasi ya nne barani Afrika kwenye masuala ya usalama wa anga
"Kadhalika uwanja wetu wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere umefanikiwa kushinda Tuzo ya Usalama ya Baraza la Viwanja vya Ndege Duniani, katika viwanja vyenye miruko ya ndege 50000 kwa mwaka.”

“Shirika pia linatarajia kuongea safari zake katika miji ya London, Lagos, Accra, Juba, Muscat na maeneo mengine ya masoko ya kimkakati ili kuiunganisha Tanzania Kikanda na Kimataifa.”
Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa mkutano huo Inatoa jukwaa adimu linalowaleta pamoja viongozi na wasimamizi wa usafiri wa anga, waendeshaji wa viwanja vya ndege kujadili na kubadilishana mawazo katika kuboresha na kuikuza sekta ya usafiri wa Anga.
