Hii hapa, Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la Mwaka 2024)

KUFUATIA kuzaliwa kwake baada muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kuwa Jamhuri Moja iliyoungana na yenye Mamlaka kamili mnamo mwaka 1964, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) ilifafanua maudhui, namna ya kuyaainisha na utaratibu wa kuendesha uhusiano wa kimataifa ili kuongoza ushiriki wake katika ushirikiano wa uwili, kikanda na kimataifa.

Uendeshaji wa masuala ya kigeni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulijikita katika misingi ya kutofungamana na upande wowote, umoja wa Afrika, uhuru, usawa, kufungamana kwa masilahi nchi huru , na kuheshimu utu na haki za binadamu.

Misingi hii imejenga msingi wa uanzishwaji wa uhusiano wa kirafiki na nchi nyingine sambamba na mashirika ya kikanda na ya kimataifa. Vilevile, Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliathiriwa na msingi wa kisiasa wa haki ya Waafrika kujitawala wenyewe.

Sera hii iliongoza harakati za ukombozi wa maeneo ya Afrika yaliyokuwa chini ya utawala wa kikoloni, ukombozi wa watu waliodhulumiwa, na kuendeleza umoja wa Afrika.

Kwa muktadha huo,utekelezaji wa masuala yanayohusu uhusiano wa kimataifa uliongozwa na Waraka wa Rais Namba 2 wa Mwaka 1964, Azimio la Arusha la mwaka 1967 na Sera Mpya wa Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, ikiwa ni pamoja na misingi ya kimataifa iliyomo kwenye Mikataba ya Vienna ya mwaka 1961 na 1963 mtawalia.

Hivyo, Sera Mpya ya Mambo ya Nje iliundwa ili kukabiliana na mabadiliko ya kitaifa, kikanda na kimataifa ambayo yalianza kujitokeza katikati mwa miaka ya 1980, ikiwemo uhitaji wa kufungamana na mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, pamoja na kuongezeka kwa kasi ya utandawazi.Endelea...


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news