ABIDJAN-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza jambo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), kando ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2025 ambao utakuwa wa 60 wa Bodi ya Magavana wa ADB na wa 51 kwa ADF ulioanza Mei 26 hadi 30 Mei 2025 katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Abidjan, Côte d’Ivoire, na utajumuisha uchaguzi wa Rais na Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi hiyo baada ya Rais wake wa sasa, Dkt. Akwinumi Adesina, kumaliza muda wake.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya AfDB ambayo ni tukio muhimu zaidi la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya AfDB ambayo ni tukio muhimu zaidi la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).Hutoa fursa kwa Kundi la Benki – likijumuisha Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Mfuko wa Maendeleo ya Afrika (ADF), na Mfuko Maalum wa Nigeria kufanya tathmini ya maendeleo ya mwaka uliopita pamoja na wanahisa.
Pia ni jukwaa mahsusi kwa viongozi wa serikali na washiriki wengine, wakiwemo waandishi wa habari, kujadili masuala muhimu ya maendeleo ya Afrika.Zaidi ya wajumbe 6,000 wanatarajiwa kuhudhuria, wakiwemo Marais na Wakuu wa Serikali za Afrika, Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Mabenki Kuu, washirika wa maendeleo, wawakilishi wa sekta binafsi, viongozi wa asasi za kiraia, wasomi, taasisi za utafiti, NGOs, na wadau wengine.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Kufanya Rasilimali za Afrika Kufanya Kazi kwa Maendeleo ya Afrika".
Lengo ni kutambua na kutumia rasilimali mbalimbali za Afrika ikiwemo watu, maliasili, fedha, na biashara kwa ajili ya mabadiliko ya kimuundo ya bara hili.
Malengo ni kukuza uchumi jumuishi, wa kijani na wenye ustahimilivu, huku yakihamasisha ushirikiano wa kimataifa wa kifedha.
Mkutano pia utajadili masuala mtambuka kama mageuzi ya kidijitali, uimarishaji wa taasisi na utawala bora.
Haya yote yanalingana na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi, Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika, na Mikakati Kuu Mitano ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (High 5s).
Mbali na mikutano rasmi ya Bodi ya Magavana, kutakuwa na matukio ya maarifa yaliyoandaliwa na Benki pamoja na nchi mwenyeji, Côte d’Ivoire.Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Katibu Mkuu ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba, ni miongoni mwa Magavana na Magavana Mbadala wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), mtawalia.




