Mheshimiwa Mbeki awasili Morogoro kwa ziara maalum

MOROGORO-Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki amewasili Morogoro kwa ziara maalum kutembelea eneo la kihistoria la Mazimbu, ambalo lilikua makazi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini waliokuwa uhamishoni wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Rais Mstaafu Thabo Mbeki amepanda Treni ya SGR kwa ajili ya kwenda Kutembelea Eneo la Mazimbu, Morogoro.

Katika Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete Morogoro Mheshimiwa Mbeki amelakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima na viongozi wengine wa Serikali.
Ziara hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Afrika, yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Mei, ikiwa ni kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (zamani OAU) na kuhamasisha mshikamano, maendeleo na utambulisho wa bara la Afrika.

Mheshimiwa Mbeki yuko nchini kwa mwaliko wa Taasisi ya Thabo Mbeki kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Tanzania, ambapo pamoja wameandaa maadhimisho haya ya kitaifa ya Siku ya Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news