KULINGANA na matakwa ya Kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Serikali imetoa Kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za Mwaka 2025. Aidha,kanuni hizo zimechapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 198 la Machi 28, 2025.
Kwa mujibu wa Kanuni hizo, bei na malipo ya bidhaa na huduma zote ndani ya nchi zinapaswa kufanyika kwa Shilingi ya Tanzania.
Hivyo, ni kosa kunukuu, kutangaza au kubainisha bei kwa kutumia fedha za kigeni; kulazimisha, kuwezesha au kupokea malipo kwa fedha za kigeni au kukataa malipo kwa Shilingi ya Tanzania;