Waliofaulu vizuri Samia Scholarship kusomeshwa nje ya nchi-Waziri Mkenda

DODOMA-Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Mheshimiwa Profesa Adold Mkenda amesema kuwa kupitia SAMIA SCHOLARSHIP v4ijana waliofanya mtihani wa kidato cha sita watakapochaguliwa ambao watapenda kusoma nje ya nchi wanatakiwa kukaa mwaka mmoja ambapo wataweka kambi kampasi ya Nelson Mandera Africa Institute of Teknology kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo uzalendo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelezea mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Waziri wa wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa pia watajifunza kuielewa nchi yao na namna ya kuitetea huko watakapoenda kusoma.

Amesema kuwa,Serikali itachukua kuanzia vijana 50 mpaka 100 kwa sharti la kukubali kusoma ndani ya nchi kwa mwaka mmoja ili kufundishwa uzalendo na kuwajengea uwezo kuhusu utamaduni mpya watakaokutana nao nje ya nchi.

Aidha, amesema kuwa kupitia SAMIA SCHOLARSHIP serikali imejipanga kwa ajili ya kuchukua vijana kati ya 650 mpaka 700 watakaofaulu vizuri katika masomo yao na kupata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news