Yanga SC yaangukia pua CAS, Kariakoo Derby ipo pale pale

CAIRO-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imeangukia pua katika kesi yake ya awali iliyoifungua kwenye Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS).
Ni dhidi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi (TPLB) na Simba Sports Club (Simba SC) ikiomba kupewa alama tatu na mabao tatu.

Vilevile iliitaka CAS izuie tarehe nyingine ya Kariakoo Derby isipangwe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa ikiwa siku kadhaa zimepita tangu Simba SC kugoma kucheza.

Mchezo huo ulikuwa uchezwe Machi 8, 2025 hali iliyopelekea Yanga SC kupeleka kesi hiyo CAS wakigomea mechi hiyo kuchezwa tena.

Barua ya CAS iliyotolewa Mei 1, 2025 kwenye hukumu hiyo CAS imesema haina uhalali wa kisheria wa kusikiliza kesi hiyo yenye kumbukumbu CAS 2025/A/11298.

Ni kati ya Yanga SC, Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kabla halijapitia kwenye mamlaka za kisheria za TFF,hivyo imelifuta rasmi na kuliondoa shauri hilo kwenye mfumo wake wa mashauri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news