MOROGORO-Watu tisa wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hai lenye namba za usajili T523 EKM kugongana na lori lililokuwa limebeba shehena ya sukari lenye namba za usajili T406 CZS-T804 BUB.
Ni katika eneo la Kijiji cha Lugono Melala huko Barabara Kuu ya Morogoro kuelekea mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Taarifa zaidi zitakujia hapa.
