EWURA yatangaza bei ya mafuta mwezi Juni,2025 huku yakishuka bei

DAR-Bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Juni, 2025 imeendelea kuleta nafuu kwa watumiaji wa vyombo vya moto nchini ikilinganishwa na bei za mwezi Mei, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Juni 4,2025 kwa mafuta yaliyopokelewa Bandari ya Dar es Salaam, bei ya petroli imeshuka kwa shilingi 72.16, dizeli kwa shilingi 51.89 na mafuta ya taa shilingi 184.93.

Kwa bandari ya Tanga, petroli imeshuka kwa shilingi 69.41 huku dizeli ikishuka kwa shilingi 50.1, Mtwara, petroli imeshuka kwa shilingi 71.65 na dizeli shilingi 51.37.

Aidha, bei za Juni 2025, zimeakisi kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa asilimia 0.9 ya kwa mafuta ya petroli, asilimia, 3.4 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 3.7 kwa mafuta ya taa mtawalia; hali iliyochagiza kupungua kwa bei kikomo za Juni 2025.

Vilevile, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa asilimia 0.63 huku gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam zikiwa zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 4.34 kwa mafuta ya petroli, asilimia 22.43 kwa mafuta ya dizeli na kupungua kwa asilimia 1.65.

Kwa uapande wa Bandari ya Mtwara, gharama za uagizaji zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 51.55 kwa mafuta ya petroli na hakuna mabadiliko kwenye mafuta ya dizeli.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news