IRINGA-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeendelea kuimarisha misingi ya utawala bora kwa watumishi wake kwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara yanayolenga kuongeza uadilifu, uwajibikaji na kupambana na vitendo vya rushwa katika maeneo ya kazi.
Katika muendelezo wa juhudi hizo Juni 3, 2025,TFS imekaribisha Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Iringa katika Shamba la Miti la Sao Hill kwa ajili ya kutoa elimu kwa wahifadhi kuhusu namna ya kuepuka na kupambana na rushwa, sambamba na kuimarisha maadili ya utumishi wa umma.
Akizungumza katika mafunzo hayo,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Bw. Victor Swella,* alisema elimu hiyo inalenga kuwakumbusha watumishi kuhusu wajibu wao kwa umma na kuhimiza matumizi sahihi ya madaraka waliyopewa ili kuimarisha uwajibikaji na kuondoa mianya ya rushwa.
“Kila mtumishi wa umma anapaswa kutumia madaraka aliyopewa kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria."
Tags
Habari
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Tanzania
Tanzania Forest Services (TFS)
TFS
