Mama Mariam Mwinyi aishukuru China kwa kuendelea kuisaidia ZMB

ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameihakikishia China kuwa itaendelea kushirikiana nayo kuhakikisha malengo ya kuwakomboa wanawake,vijana na watoto yanafikiwa.
Ameyasema hayo alipozungumza na Balozi Mdogo Mpya wa China anaefanyia kazi zake Zanzibar Mhe. Li Quanghua aliefika Ofisini kwake Migombani kwa kujitambulisha tarehe 27 Juni 2025.
Aidha, Mama Mariam Mwinyi ameishukuru Serikali ya China kwa kuwa mshirika wa maendeleo katika kutekeleza miradi inayolenga kuleta mabadiliko chanya katika sekta za afya, elimu, uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi hususani katika kuimarisha Kilimo cha Mwani.

Halikadhalika, Mama Mariam Mwinyi amesisitiza utayari wa ZMBF kushirikiana na China kuendeleza uhusiano wa diplomasia katika kuboresha maisha ya Wananchi wa Zanzibar.
Naye Balozi Li Quanghua ameipongeza ZBMF kwa Malengo na Mafanikio inayoyapata katika kuimarisha ustawi wa jamii , mapambano dhidi ya Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, usawa wa kijamii na kuimarisha Afya ya Mama na Mtoto pamoja na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi hususani katika kuimarisha Kilimo cha Mwani.Pia, ameahidi kuendeleza ushirikiano zaidi na ZMBF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news