Wakuu wa mikoa kuanza kuelezea mafanikio ya Serikali kuanzia Julai

DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa kuanzia Julai Mosi mwaka huu kutakua na mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Waandishi wa habari yenye lengo la kutoa taarifa kwa umma kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika mikoa wanayoiongoza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa tarehe 29 Juni, 2025 ametoa taarifa ya Serikali kupitia mkutano na Waandishi wa Habari katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara; Sabasaba, Dar es Salaam ambapo amezungumzia masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali katika kuwaletea Watanzania maendeleo.

Msigwa amesema hayo Julai 29, 2025 jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali imeandaa mikutano hiyo kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali.

"Idara ya Habari, MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali tumeratibu na kukamilisha mikutano ya Wakuu wa Taasisi, Mawaziri na vyombo vya habari na sasa tumeandaa mikutano ya Wakuu wa Mikoa wote na Waandishi wa Habari itakayofanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 01 Julai, 2025 na itakamilika tarehe 18 Julai mwaka huu.”
Kuhusu ratiba ya kuanza kwa mikutano hiyo Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema itaanza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Julai 1, 2025 ikifuatiwa na Mkoa wa Katavi Julai 3, 2025, Mkoa wa Singida Julai 4, 2025 na Mkoa wa Geita tarehe 9 Julai, 2025.

Pia ametaja mikoa mingine inayoguswa na ratiba hiyo kuwa ni Arusha, Tabora, Shinyang, Tanga, Simiyu na Mwanza ambapo katika kuelekea mikutano hiyo amewaomba wananchi wa Mikoa yote iliyotajwa wafuatilie matangazo ya moja kwa moja ya mikutano hiyo ili kujua Serikali imefanya nini katika mikoa yao.
Aidha, ameeleza kuwa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na vyombo vingine vya habari vya Redio, Televisheni, Mitandao ya Kijamii ikiwemo chaneli ya Idara ya Habari (Maelezo TV) vitarusha matangazo hayo mbashara ambayo pia yatachapishwa kwenye magazeti mbalimbali.
"Nawaomba Makatibu Tawala wa Mikoa husika waratibu ushiriki wa mikoa yao bila kukosa kama ratiba inavyoonesha. Aidha, Idara ya Habari (MAELEZO) imepita kwenye mikoa husika kuchukua picha mnato na jongefu na kufanya mahojiano na wananchi wanaonufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye Mikoa hiyo ambazo zitasambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,”amesisitiza Msigwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news