LINDI-Katika Mahakama ya Wilaya Kilwa mkoani Lindi imetolewa hukumu dhidi Mhasibu wa Chama cha Msala Mwekundu Tanzania,Bi.Carrie Chizara ya adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela.
Picha hii ni mfano, haina uhusiano na saini hizo zilizoghushiwa. (Freepik).
Ni kwa makosa ya kughushi chini ya kifungu cha 333,335(a) na 337 Penal Code na kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 R.E 2022].
Kifungu hicho kikisomwa pamoja na Aya ya 21, Jedwali la kwanza, pamoja na vifungu vya 57(1) na 60 (2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi [CAP 200 R.E 2022].
Awali ilielezwa kuwa, mshtaikiwa Bi.Carrie Chizara alishitakiwa kwa makosa matatu, kosa la 1 na 2 akiwa kama mhasibu wa mradi alighushi saini za walipwaji na kosa la tatu mshitakiwa aliwasilisha hati za malipo kwa mwajiri wake zenye saini za kughushi na kuonyesha kuwa, amewalipa wahusika huku akijua si kweli.
Hukumu dhidi ya Bi.Carrie Chizara imetolewa Mei 30, 2025 kutokana na shauri la uhujumu uchumi Na. 21226/2024 lililokua mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Bi.Caroline Mtuhi, shauri ambalo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi,Bw. Gregory Chisauche.
