MBEYA-Katika Mahakama ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Neema Christopher, imefunguliwa shauri la jinai namba 14859/2025, Jamhuri dhidi ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Lualaje Bw. Matatizo Kubelo Mwambipile.
Mshtakiwa anashtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa chini ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.Mshtakiwa alikuwa ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya katika nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Lualaje kilichopo Kata ya Lualaje
Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU,Kissa Ngoloke, Juni 18, 2025 alisema mshtakiwa aliomba na kupokea rushwa ya kiasi cha sh.800,000 ili aweze kumsaidia mwanakijiji mmoja kumpatia sehemu ya shamba la kijiji, hivyo kuisababishia hasara halmashauri hiyo kiasi cha shilingi 800,000.
Mshtakiwa amekubali kutenda kosa hilo na kutiwa hatiani na kuhukumiwa kulipa faini ya 500,000 au kutumikia kifungo cha miaka 3 jela.
Pia ameamriwa kurejesha sh.800,000 aliyopokea kwa njia za rushwa. Mshtakiwa amelipa faini ya sh.500,000 na amerejesha sh. 800,000.
Tags
Habari
Mahakamani Leo
Programu Rafiki ya TAKUKURU
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)