ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya barabarani iliyotokea Juni 7, 2025 katika eneo la Mlima Iwambi, mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya watu 28, wakiwemo wanawake, watoto, pamoja na kujeruhi wengine.
Kwa niaba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wote waliopoteza maisha katika ajali hiyo, sambamba na kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurejea katika afya njema.
Katika salamu hizo za pole, Rais Dkt. Mwinyi amewasihi wote walioguswa na msiba huo kuwa na subira na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
Rais Dkt. Mwinyi amewaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amin
Hakika sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

