DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe.George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Mhe. Masaju anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye amestaafu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 13, 2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka ambapo imeeleza kuwa, uapisho wa Jaji Mkuu utafanyika tarehe 15 Juni, 2025 Ikulu, Chamwino Dodoma kuanzia saa 4.00 asubuhi.
