DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 01, 2025 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan katika tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa zinazoandaliwa na Baraza la Michezo Taifa (BMT).
Lengo la tuzo hizo ambazo zitafanyika katika Ukumbi wa Superdome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam ni kuwaenzi na kuwatambua watanzania wanaiowakilisha nchi katika michezo mbalimbali duniani na kuiletea sifa Tanzania kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

Katika hafla hiyo Mheshimiwa Majaliwa alipokea kwa niaba ya Rais Dkt. Samia tuzo ya kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia alikabidhiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kusimamia michezo nchini.