KILIMANJARO-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Za Kulevya (DCEA) Kanda Ya Kaskazini kwa kushirikiana na Serikali ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imetoa mafunzo maalum kwa viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi vitongoji.
Lengo likiwa ni kukabiliana na adhari zitokanazo na dawa za kulevya aina ya mirungi pamoja na kuwajulisha viongozi hao kuwepo kwa mkakati wa pamoja wa Serikali wa kuhamasisha mazao mbadala.Ni katika kukabiliana na kilimo cha dawa za kukevya aina ya mirungi katika Kata za Vudee, Tae,Gavao Saweni pamoja na maeneo mengine.
Mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na washiriki zaidi ya 80 imewahusisha viongozi kutoka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Same, Waheshimiwa Madiwani, viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Watendaji ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji kutoka Kata za Vudee, Tae na Gavao Saweni ambapo mgeni rasmi katika mafunzo hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)





