Serikali yafanikiwa kudhoofisha mitandao ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema,Serikali imeimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kupunguza uingizaji, uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini.

Ni kwa kubaini na kudhoofisha mitandao ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambapo jukumu hilo huwa linatekelezwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikin na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Ameyasema hayo Juni 27,2025 wakati wa hotuba ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

"Katika kipindi hiki, tulikamata jumla ya Kilogramu 4,697,511.35 za dawa za kulevya zikihusisha watuhumiwa 25,715.

"Kwa upande mwingine, katika kuwasaidia waathirika, tumeongeza vituo vya utoaji huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya kutoka vituo tisa mwaka 2020 hadi 18 mwaka 2025, ili kupanua wigo wa huduma hii muhimu.

"Pamoja na hatua hizo, hatua nyingine madhubuti za kudhibiti na kuwalinda vijana wetu dhidi ya dawa hizo zinaendelea kuchukuliwa."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news