Ustawi na maendeleo ya watoto,vijana ni nguzo muhimu nchini-Dkt.Jingu

NA GODFREY NNKO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema,ustawi na maendeleo ya watoto na vijana ni jambo muhimu katika Taifa na jamii kwa ujumla.
Dkt.Jingu ameyasema hayo leo Juni 9,2025 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kutangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili dhidi ya Watoto na Vijana Tanzania (VACS-2024).

"Na kwa kweli,leo na kesho na Taifa lolote linategemewa na jinsi ambavyo Taifa,jamii inashughulikia masuala ya ustawi wa maendeleo ya watoto."

Dkt.Jingu amebainisha kuwa, Tanzania ikiongozwa na viongozi wakuu Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi wamewekeza zaidi katika ustawi wa jamii.

"Ndiyo maana tunaona wameamua kuunda wizara maalum kabisa zinazoshughulia masuala ya ustawi na maendeleo ya watoto na vijana."

Amesema,Serikali imeweka mkazo na imewekeza zaidi katika kuhakikisha ustawi na maendeleo ya watoto yanapewa uzito mkubwa.

"Ili kuhakikisha watoto wanalelewa vizuri, wanakuwa vizuri, wanatunzwa vizuri ili baadae wakikuwa waweze kutengeneza maisha na familia zao vizuri."

Ingawa Dkt.Jingu anaweka wazi kuwa, kazi hiyo ya Serikali kupitia wizara husika haiwezi kufanya pekee bali ni kupitia ushirikiano na wananchi wenyewe wakiwemo wadau mbalimbali.

Hivyo, Dkt.Jingu anabainisha kuwa, wizara zao zinaratibu juhudi za wadau kama walivyoshirikiana kufanya utafiti wa Kitaifa wa ukatili dhidi ya watoto na vijana nchini 2024.

Miongoni mwa wadau walioshiriki katika utafiti huo, Dkt.Jingu amewataja kuwa ni PEPFAR na CDC za Marekani, Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Pia,wadau kutoka sekta binafsi ikiwemo Tanzania Health Promotion Support (THPS) huku taasisi bobezi za Serikali zikisimamia utafiti huo.

Amezitaja taasisi hizo kuwa ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar (OCGS) na wengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news