BEIJING-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewasili Beijing, China tarehe 9 Juni, 2025 kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Kiongozi wa Ngazi ya Juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri wa Watu wa China, Bw. Xu Zhongsheng pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, Mhe. Khamis Mussa Omar.

Aidha, pembezoni mwa mkutano huo Waziri Kombo atafanya mazungumzo na Mheshimiwa Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) na Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya Tanzania na China.
Vilevile, Waziri Kombo na ujumbe wake watatembelea majimbo ya Sichuan na Shenzhen, ambapo watakutana na viongozi wa mikoa hiyo pamoja na kampuni mashuhuri za biashara na uwekezaji za China. Mikutano hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na China, hasa katika masuala ya kisiasa na kiuchumi na kuhamasisha kampuni za China kuja kuwekeza nchini.