SINGIDA-Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imetumia shilingi bilioni 6.361 kujenga shule mpya sita za sekondari.
Vilevile, shule sita zimefanyiwa ujenzi wa upanuzi wa miundombinu ya kidato cha 5 na 6, ujenzi wa vyoo na nyumba za walimu katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Akitoa taarifa ya miradi ya elimu iliyojengwa katika Wilaya ya Iramba, Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mhe. Suleiman Mwenda amesema kuwa,ujenzi wa shule hizo utaimarisha sekta ya elimu ikiwemo kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Amezitaja shule hizo zilizojengwa wilayani hapo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Maluga uliogharimu shilingi milioni 470.Ujenzi wa Shule ya Sekondari Ndulungu uliogharimu shilingi milioni 470,ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mtoa Darajani uliogharimu shilingi milioni 544.225.
Miradi mingine mipya ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Makunda uliogharimu shilingi milioni 544.225.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kizega uliogharimu shilingi milioni 544.225 na ujenzi wa Shule ya Sekondari Amali Kitukutu uliogharimu shilingi bilioni 1.6.
Pia,ujenzi wa vyoo matundu tisa Shule ya Sekondari Mtoa kwa gharama ya shilingi milioni 15.3 na ujenzi wa vyoo matundu tisa katika Shule ya Sekondari Shelui kwa gharama ya shilingi milioni 15.3.
Katika hatua nyingine,DC Mwenda ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kwa weledi ujenzi wa nyumba moja ya mwalimu (2 in 1) katika Shule ya Sekondari Maluga kwa gharama ya shilingi milioni 110.
Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika Shule ya Sekondari Ndulungu kwa gharama ya shilingi milioni 110, na Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika Shule ya Sekondari Iramba kwa gharama ya shilingi milioni 95.
Kuhusu ujenzi wa upanuzi wa miundombinu ya kidato cha 5 na 6, Mhe.Mwenda amesema kuwa, jumla ya shule sita zimepata miundombinu hiyo ikiwemo Shule ya Sekondari Lulumba iliyopata kiasi cha shilingi milioni 352.8, Shule ya Sekondari Tumaini shilingi milioni 252.4.
.jpg)
.jpg)





