DODOMA-Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele amesema,Agosti 28 hadi Oktoba 27, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za Urais, Wabunge na Madiwani kwa Tanzania Bara na Zanzibar na Jumatano Oktoba 29,2025 ndio itakuwa siku ya kupiga kura.
Jaji Mwambegele ameyasema hayo leo Julai 26,2025 jijini Dodoma wakati akitangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Amesema, Agosti 9 hadi Agosti 27, 2025 itakuwa ni kipindi cha kutoa fomu za uteuzi wa Wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais na Agosti 27, 2025 itakuwa siku ya uteuzi wa Wagombea wa kiti cha Rais, Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani.
