Maandalizi ya hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Dira 2050) yakamilika

DODOMA-Maandalizi ya hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Dira 2050) yamekamilika ambapo uzinduzi wa Dira hiyo utafanyika tarehe 17 Julai 2025.
Uzinduzi huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete, Dodoma, Mgeni Rasmi atakuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Meneja wa Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), maandalizi ya uzinduzii wa Dira 2050 yamekamilika.

Uzinduzi wa Dira 2050 unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wananchi 5,000 kutoka sehemu mbalimbli ndani na ncje ya nje.

Tukumbuke kuwa maandalizi ya Dira 2050 yalishirikisha wadau mbalimbali waliotoa maoni yao kuhusu Tanzania wanayoitaka ifikapo mwaka 2050.

Maoni hayo ndiyo msingi wa Dira 2050 itakayozinduliwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news