Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Samia Suluhu AFCON Arusha umefikia asilimia 51, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 yatakayofanyika nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenan Kihongosi ameyasema hayo Julai 20,2025 jijini Dodoma wakati akiwasilisha mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo mbele ya waandishi wa habari.
Kihongosi amesema,Serikali imetumia shilingi bilioni 298 kufanikisha ujenzi huo kama sehemu ya mkakati wa kukuza sekta ya michezo na utalii, huku uwanja huo ukitarajiwa kuwa kivutio kikubwa cha kimataifa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























