Waziri Mkuu aelekea Belarus kwa ziara ya kikazi

DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 20, 2025 ameondoka nchini kuelekea nchini Belarus kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu. Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kukuza fursa za kiuchumi kati ya Tanzania na Belarus.
Katika ziara hiyo, Mhe. Majaliwa anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Belarus, Alexander Turchin ambapo watajadili masuala ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu,kilimo na viwanda.

Waziri Mkuu pia atapata fursa ya kutembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa nchini humo cha Republican Unitary Production Enterprise na kujionea mbinu za kisasa za uzalishaji wa bidhaa za afya.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia atatembelea kiwanda cha matrekta cha Minsk Tractor Works JSC pamoja na chuo kikuu cha Agrarian State University.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kufanya mikutano ya uwili itakayojumuisha viongozi wa kiserikali na Chama cha wafanyabiashara wa Belarus cha AFTRADE.

Lengo la mikutano hiyo ni kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kuvutia wawekezaji kutoka Belarus kuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta za kimkakati.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Cosato Chumi, Katibu Mkuu Wizaya Nishati Mhandi Felchesmi Mramba pamoja Naibu Katibu Mkuu Kilimo Dkt. Stephen Nindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news