Rais Dkt.Samia ateua viongozi 10 leo

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

(i) Bw. Omari Juma Mkangama ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa;

(ii) Bw. Juma Abdallah Njeru ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda;

(iii) Bi. Hellen Emmanuel Mwambeta ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha;

(iv) Bw. Francis Genes Kafuku ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu;

(v) Dkt. Adam Omar Karia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Maji kwa kipindi cha pili;

(vi) Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA);

(vii) Jenerali Mstaafu Venance Salvatory Mabeyo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro
kwa kipindi cha pili.

(viii) Dkt. Harrison George Mwakyembe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kipindi cha pili;

w. Filbert Michael Mponzi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Sukari Tanzania kwa kipindi cha pili; na

(x) Dkt. Leonada Raphael Mwagike ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kipindi cha pili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news