DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 8,2025 Ikulu jijini Dar Es Salaam amepokea Tuzo Maalum ya Power of 100 Women Award kutoka kwa Uongozi wa Access Bank Group ambapo amekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Access Tanzania,ndugu Protase Ishengoma.

Tuzo hii ambayo hutolewa kila baada ya miaka mitano inalenga kutambua na kusherehekea wanawake wa Kiafrika wanaotoa michango ya mageuzi kwa mataifa na jamii zao, kuhamasisha na kuhimiza kizazi kijacho cha viongozi Wanawake katika bara zima la Afrika.
Pia kupaza sauti za Wanawake katika kuleta maendeleo endelevu ya Kiuchumi na kijamii barani Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Tuzo Maalum ya ‘Power of 100 Women Award mara baada ya kukabidhiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam 08 Julai, 2025.




