DAR-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 27 wa Kamati ya Mawaziri ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (MCO).
Mkutano wa Mawaziri umepangwa kufanyika kuanzia Julai 21 hadi 25, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkutano huu wa ngazi ya juu unalenga kuwaleta pamoja wadau wakuu kujadili na kushughulikia masuala ya kikanda yanayohusiana na siasa, ulinzi na ushirikiano wa kiusalama katika kanda ya SADC.
.jpeg)

