ALGIERS-Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Bw. Crispin Francis Chalamila, ameungana na Wakuu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa barani Afrika, kuadhimisha Siku ya Kupambana na Rushwa inayoadhimishwa mjini Algiers nchini Algeria.
Wakuu hawa ambao wako Algiers, wanashiriki maadhimisho haya kupitia 'Associstion of African Anti - Corruption Authorities - AAACA', ambao pamoja na mambo mengine watakuwa na Mkutano Mkuu wa 7 wa Mwaka wa Shirikisho hilo,Julai 21 na 22, 2025.Maadhimisho haya yanafanyika nchini Algeria katika ukumbi wa 'International Conference Center - Abdelatif Rahal, Algiers - Algeria' na kuhudhuriwa na washiriki takriban 250 wakiwemo viongozi kutoka nchi 28 za Afrika.