Wananchi waendelea kumiminika banda la BoT maonesho ya Sabasaba kupata elimu

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inashiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 14 Julai 2025.
Katika maonesho haya, BoT inatoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa sera ya fedha na mchango wake katika kudhibiti mfumuko wa bei na kuimarisha uchumi wa nchi, pamoja na namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali za muda mfupi na muda mrefu.
Pia, elimu inatolewa kuhusu mifumo ya malipo ya taifa inayowezesha miamala kufanyika kwa haraka na usalama, sambamba na namna ambavyo BoT inasimamia sekta ya fedha ili kuhakikisha taasisi za kifedha zinafanya kazi kwa ufanisi na kwa mujibu wa sheria.
Vilevile, wananchi wanaelimishwa kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa huduma za kifedha, masuala ya ajira na utumishi ndani ya Benki Kuu, pamoja na fursa za masomo zinazotolewa na Chuo cha BoT kwa wanaotaka kujijengea ujuzi katika masuala ya fedha na kibenki.
Aidha, BoT inatoa elimu maalumu kuhusu namna ya kutambua alama za usalama katika noti za Tanzania na njia sahihi za kutunza noti na sarafu ili kudumisha ubora na matumizi salama ya fedha taslimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news