Waziri Sarai ahimiza usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano

DAR-Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada, Mhe. Randeep Sarai amesema kuwa, usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ni haki ya msingi inayopaswa kutekelezwa kwa wakati, ili kuwapa watoto haki zao na kutokuathiri mustakabali wa maisha yao.
Mhe. Sarai ameyasema hayo alipotembelea Kituo cha Afya cha Makuburi cha jijini Dar Es Salaam kukagua maendeleo na utekelezaji wa program za huduma za afya zinazofadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Programu hizo ni pamoja na Usajili wa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto Chini ya Miaka Mitano ambayo imeleta mafanikio makubwa, pamoja na ile ya utoaji huduma ya matone ya Vitamin A kwa watoto wa miezi sita hadi miaka 5.
Mheshimiwa Sarai ameeleza kuwa, cheti cha kuzaliwa hutoa msingi wa utambulisho wa mtoto, kinamwezesha kupata jina, uraia na kufikiwa na huduma muhimu za kijamii kama vile afya, elimu na ulinzi.

Aidha, ameongeza kuwa ufadhili kutoka Serikali ya Canada kupitia Shirika la Kimataifa la Nutrition International umeiwezesha Tanzania kuvuka lengo la kusajili watoto milioni saba mwaka 2013, ambapo jumla ya watoto milioni 11 walisajiliwa, hatua amesema inastahili pongezi kwa Serikali ya Tanzania.
Ameongeza kuwa ufadhili wa Canada kupitia Shirika la Kimataifa la Nutrition International umeiwezesha Tanzania kuvuka lengo la kusajili watoto milioni saba kwa mwaka 2013, ambapo watoto milioni 11 walisajiliwa, na kutoa pongezi kwa Serikali ya Tanzania.

"Naipongeza Tanzania kwa mara nyingine tena kwa mafanikio makubwa iliyoyapata mwaka huu, kwa kufanikisha utoaji wa matone ya Vitamini A kwa asilimia 90 kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi miezi 59. Mafanikio haya yamechangia kudhibiti ongezeko la magonjwa ya kuambukiza kwa watoto, yakiwemo surua na kuharisha," alisema Mhe. Sarai.
Mjumbe wa Bodi ya Nutrition International na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ameishukuru Canada kwa kuchangia maendeleo ya sekta ya afya, hususan kupitia huduma ya utoaji wa matone ya vitamini A kwa Watoto, kwani imewezesha kujenga taifa lenye afya bora kwa maendeleo endelevu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news