ARUSHA-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ametembelea banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Kongamano la Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Taasisi za Umma linaloendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.
Katika banda hilo, Mheshimiwa Dkt.Mpango amepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw.Hamad Abdallah ambaye amemuelezea kuhusu huduma na miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika ikiwemo ile ya kimkakati nchini.





