EWURA yatangaza bei ya mafuta kwa mwezi Agosti,2025

DAR-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za petroli zitakazotumika hapa nchini kuanzia Jumatano ya Agosti 6, 2025, zikionesha kupungua kwa bei ya petroli kwa shilingi 34 kwa mafuta yaliyopokelewa Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile imeeleza kuwa,bei ya petroli katika soko la dunia imepungua kwa asilimia 2.3 huku dizeli ikiongezeka kwa asilimia 5.7 na mafuta ya taa kwa asilimia 3.7.

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa viwango vya kubadilisha fedha,kwa bei za mwezi Agosti, 2025, wastani wa gharama za kubadilidha za kigemi umepungua kwa asilimia mbili.

Kwa upande wa ghama za kuagiza mafuta, kwa Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa wastani wa asilimia 12.3 kwa petroli, asilimia 3.11kwa dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa asilimia 13.08 huku Bandari ya Tanga kukiwa hakuna mabadiliko.

Vilevile kwa Bandari ya Mtwara, gharama zimeongezeka kwa asilimia 6.12 kwa mafuta ya petroli na asilimia 60.82 kwa dizeli.

EWURA imewakumbusha wafanyabiashara kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka agizo hilo;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news