DAR-Katika mchezo wake wa pili, Taifa Stars ya Tanzania dhidi ya Mauritania, umemalizika kwa kutikisa nyavu za mpinzani wake na kujipatia ushindi wa goli moja bila huku ikiwa inaongoza kundi B wakiwa na alama sita.
Goli hilo pekee limefungwa katika dakika ya 89 na Shomari Kapombe baada ya kupewa pasi nzuri na kuachia shuti kali lililompata golikipa wa Mauritania na kushindwa kulihimili.
Stars walionesha mchezo wa kujiamini tangu dakika ya mwanzo, wakimiliki sehemu kubwa ya mpira na kuwalazimisha wageni kucheza kwa tahadhari.Mipango ya kocha Hemed Suleiman Ali (Morocco) imeonekana kuzaa matunda, huku ikileta matumaini ya Kombe la CHAN 2024 kubaki nyumbani.
Aidha, Mudathir Yahya, amekuwa mchezaji bora wa mechi hii ya pili kwa Taifa Stars.

