TIMU ya Taifa ya soka ya Tanzania ya Taifa Stars, imemaliza mechi zake za makundi fainali za CHAN 2024 kwa kutoka 0-0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo Taifa Stars imemaliza Kundi B ikiongoza ikiwa na pointi 10, baada ya kushinda michezo mitatu ya mwanzo.Madagascar imeshika nafasi ya pili ikiungana na Stars kucheza robo fainali baada ya kuifunga Burkina Faso mabao 2-1, hivyo kufikisha pointi 7 sawa na Mauritania isipokuwa Madagascar ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













