DAR-Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa taarifa kwa umma kuhusu kubaini uwepo wa Dettol za maji bandia zenye ujazo tofauti, ambazo zinatengenezwa kinyume cha sheria.
Uhalifu huu ulibainika baada ya taarifa za kiintelijensia zilizopelekea ukaguzi wa pamoja na Jeshi la Polisi katika nyumba ya kulala wageni ya New Kishimbe Lodge, iliyopo Mtaa wa Namanga, Kahama Mjini Mkoa wa Shinyanga.
Katika ukaguzi huo, TMDA na Polisi walikuta malighafi mbalimbali zikiwemo chupa tupu, lebo, rangi, na kemikali, katika chumba walichokuwa wakiishi watuhumiwa wawili kutoka nchi jirani.
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.



