NJOMBE-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe imefungua kesi ya Uhujumu Uchumi Na.Ecc 19436/2024 mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Njombe, Mhe.Matilda Kayombo dhidi ya Bw. Jackson Sindoma Magebe ambaye ni mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi na mmiliki wa kampuni ya J2 Investment Campany iliyopo Dar es Salaam.
Mshatakiwa ameshtakiwa kwa kutenda kosa la kutumia nyaraka kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha PCCA kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kughushi nyaraka.Kosa hilo ni kinyume na Kifungu cha 333,335(a) 307 na 337 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16, Marejeo ya Mwaka 2022 na Kuisababishia Mamlaka hasara Kinyume na Vifungu 57(1) na (4) Jedwali la Kwanza vya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Kupangwa Sura ya 200 ilifanyiwa Marejeo Mwaka 2022.
Aidha mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake, alikanusha mashtaka yote manne.Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana mpaka Agosti 21,2025 shauri hilo litakapotajwa tena .
Tags
Habari
Mahakamani Leo
PCCB Tanzania
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU