ARUSHA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ametembelea banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Kongamano la Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Taasisi za Umma linaloendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah, aliongoza maonesho ya huduma na fursa mbalimbali zinazotolewa na shirika, zikivutia viongozi na wadau wa sekta ya fedha na umma.
Kongamano hili linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, na limewaleta pamoja viongozi wa mashirika ya umma, wenyeviti wa bodi na watunga sera, kwa lengo la kujadili mbinu za kuimarisha taasisi za umma na mchango wake katika maendeleo ya Taifa.



