ACCRA-Mawaziri wa Ulinzi na Mazingira wa Ghana wamefariki katika ajali ya Helikopta ya Kijeshi katika eneo la kati la Ashanti, pamoja na watu wengine sita.
Julius Debrah ambaye ni Mkuu wa Majeshi amewaeleza waandishi wa habari kuwa,Waziri wa Ulinzi Edward Omane Boamah na Waziri wa Mazingira, Sayansi na Teknolojia,Ibrahim Murtala Muhammed (50) wamefariki katika ajali hiyo ambayo amesema ni pigo kubwa kwa Taifa hilo.Helikopta hiyo imeondoka katika mji mkuu wa Accra, saa 09:12 kwa saa za huko na ilikuwa inaelekea katika mji wa uchimbaji dhahabu wa Obuasi.