Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe. Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Shoka Khamis Juma (kushoto) alichukua fomu hizo Agosti 14,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27, mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Shoka Khamis Juma (kushoto) wakionesha begi la fomu za uteuzi.
Wagombea wakielekezwa namna ya kujaza kitabu cha kuchukua fomu.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe akisaini fomu za uteuzi.
Mgombea Mwenza, Mhe. Shoka Khamis Juma akisaini kitabu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza.