Rais Dkt.Samia aagiza watumishi wa umma kushiriki SHIMIWI 2025

DAR-Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wa umma kushiriki kwenye michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), ili kujiepusha na magonjwa nyemelezi.
Mhe. Rais ametoa kauli hiyo Agosti 14, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa kwenye hafla ya kutunukiwa Nishani ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo ya Majeshi Kimatiafa (The Grand Cordon-CISM).
Amesisitiza kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ishirikiane na wizara zote nchini kuhimiza mazoezi sambamba na programu za kukuza vipaji.

“Hapa kuna yale mashindano yanayoshirikisha watumishi wa umma sijui yanaitwajwe SHIMIWI eeeeh na mawizara hawashiriki, sasa nikutake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo uwatake mawizara na mashirika kushiriki mashindano yale,” amesisitiza Mhe. Rais.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya kutunukiwa Nishani ya CISM kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salam tarehe 14 Agosti, 2025.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya kutunukiwa Nishani ya CISM kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 14 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipewa Tuzo ya Heshima ya Uanachama wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (Honorary Member) na Makamu wa Rais wa CISM Kanda ya Afrika, Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 14 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Nishani ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (The Grand Cordon) na Makamu wa Rais wa CISM Kanda ya Afrika Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 14 Agosti, 2025.
Pia, amesisitiza kutaka taifa letu kuwa na uwakilishi thabiti kwenye mashindano mbalimbali Kimataifa na kuwa balozi wa amani.

Michezo ya SHIMIWI mwaka huu 2025 inatarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 1 hadi 16, Septemba, kwa kushirikisha michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, mbio za baiskeli, riadha, karata, bao, draft na darts.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news