Mheshimiwa Pinda atembelea eneo la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) maonesho ya Nananane

DODOMA-Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Mizengo Peter Pinda leo Agosti 7,2025 ametembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Mhe. Pinda amepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume,ndugu Raymond Mndolwa, ambaye alieleza kwa kina kuhusu majukumu ya Tume na juhudi zinazoendelea lengo likiwa ni katika kuhakikisha Taifa linakuwa na kilimo cha uhakika kupitia matumizi bora ya miundombinu ya umwagiliaji.
Katika eneo hilo, Mhe.Pinda ametembelea shamba la mfano la tume lenye miundombinu mbalimbali ya kisasa ya umwagiliaji.

Ameelezwa namna miundombinu hiyo inavyoweza kumsaidia mkulima hususani mdogo kupanga kwa ufanisi ratiba ya umwagiliaji kulingana na mahitaji halisi ya mazao, hivyo kuongeza uzalishaji.
Mhe. Pinda alielezea kuridhishwa kwake na kazi inayofanywa na Tume na kuipongeza kwa mchango wake mkubwa katika kuboresha sekta ya kilimo kupitia mifumo ya kisasa ya umwagiliaji, ambayo inalenga kuongeza tija kwa mkulima na kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news