ARUSHA-Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah, ametembelea mabanda ya taasisi na mabenki mbalimbali, ikiwemo TCB Bank, katika Kongamano la Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Taasisi za Umma linaloendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.
Kongamano hili linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Kupitia ushiriki wake, NHC inalenga kuimarisha ushirikiano na taasisi nyingine za umma pamoja na wadau wa sekta ya fedha, ili kuongeza ubunifu, ufanisi na upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Kongamano hili limewaleta pamoja viongozi na watunga sera kwa ajili ya kujadili mbinu za kuimarisha taasisi za umma na mchango wake katika maendeleo ya Taifa.





