DAR-Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania ya Taifa Stars, imemaliza mechi zake za makundi fainali za CHAN2024 kwa kutoka 0-0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati mchezo uliomalizika usiku wa Agosti 16,2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo Taifa Stars imemaliza Kundi B ikiongoza ikiwa na pointi 10, baada ya kushinda michezo mitatu ya mwanzo.
Madagascar imeshika nafasi ya pili ikiungana na Stars kucheza robo fainali baada ya kuifunga Burkina Faso mabao 2-1, hivyo kufikisha pointi 7 sawa na Mauritania isipokuwa Madagascar ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
MSIMAMO KUNDI B
1. 🇹🇿 Tanzania-pointi 10
2. 🇲🇬 Madagascar-pointi 7
3. 🇲🇷 Mauritania-pointi 7
4. 🇧🇫 Burkina Faso-pointi 3
5. 🇨🇫 Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR)-pointi 1

















