DAR-Wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini wametembelea Makumbusho ya Benki Kuu ya Tanzania iliyopo katika ofisi za Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, wanafunzi hao walipata fursa ya kujifunza kuhusu historia ya fedha ya Tanzania,mabadiliko ya majukumu ya Benki Kuu tangu kuanzishwa kwake hadi sasa pamoja na mageuzi mbalimbali yaliyofanyika katika sekta ya fedha nchini.
Makumbusho hii itakuwa wazi siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi saa 9:00 Alasiri. Benki Kuu inawakaribisha wananchi wanaopenda kutembelea makumbusho hii kuwasilisha maombi yao kupitia barua pepe C_DEPT_STAFF@bot.go.tz




