Waandishi wa habari wahakikishiwa usalama kipindi cha uchaguzi na baada uchaguzi

NA AHMAD MMOW

WAANDISHI wa habari wametakiwa kutokuwa na hofu na usalama wao katika kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Hakikisho hilo kwa waaandishi wa habari limetolewa leo Agosti 29,2025 jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillius Wambura alipofungua mdahalo wa kitaifa kuhusu ulinzi na usalama wa waandishi.

Kamanda Wambura amesema, usalama wa waandishi ni mkubwa na wasiwe na hofu ya usalama na ulinzi katika kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Amesema,jeshi hilo linafahamu vema wajibu wake wakulinda raia na mali zao. Ikiwamo waandishi wa habari. 

Bali waandishi nao wazingatie sheria, taratibu na miongozo ya kazi zao. Huku akibainisha kwamba iwapo watatimiza wajibu wao kwa kuzingatia mambo hayo hakuna atakae waingilia na kuwazuia kutekeleza wajibu wao.

"Mimi ninaposema ni agizo, walio chini yangu wanasikia na wanatekeleza. Kwahiyo waandishi msiwe na hofu na usalama wenu," alisisitiza kamanda Wambura.

Aidha, mkuu huyo wa jeshi la polisi amesema jeshi hilo litaendelea kushirikiana kwa karibu na waandishi wa habari na wadau wengine ili kushauriana na kujadiliana kwa lengo la kupata utatuzi wa changamoto zinazoweza kujitokeza.

Kamanda Wambura aliweka wazi kwamba hakuna haja wala sababu ya kulaumiana na kunyoosheana vidole pindi inapotokea changamoto badala ya kushirikiana kutatua.

Aliadharisha pia kwakusema jukumu la ulinzi na usalama sio la vyombo vya ulinzi pekee, bali wananchi wote. Huku akiwaasa wananchi na waandishi hao watambue umuhimu wa amani na usalama wanchi.

Kwa upande wake mratibu Kituo cha Utetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRD), Onesmo Ole Ngurumwa alisema licha ya waandishi wa habari kuwa na umuhimu mkubwa. Lakini kuna nyakakati wanakutana na ugumu katika kutekeleza majukumu yao. Ikiwamo kukamatwa na kuzuiwa kutekeleza majukumu yao.

Amesema, waandishi ndio wanaovusha taarifa kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Kwahiyo usalama wao ni jambo muhimu.

Ole Ngurumwa pia aliwaasa waandishi wa habari kusimamia maadili ya taaluma yao ili kutengenezea uhakika wa usalama wao. Kwani kusimamia na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili kutasababisha wasimame kati bila kupendelea upande wowote.

Naye mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini(Union of Tanzania Press Clubs/UTPC), Kenneth Simbaya alisema hali ya sasa inatoa matumaini kwamba waandishi watafanya kazi kwa uhuru na bila kubughuziwa. Kwani ushirikiano wa waandishi na vyombo vya ulinzi, hasa jeshi la polisi ni mkubwa na mzuri.

Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha makatibu na waratibu wa vilabu vya waandishi wa habari vya mikoa ya Lindi, Pwani, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara na Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news